Chama Cha Wanawake Wajane Tanzania (CCWWT)

  • ccwwtz@gmail.com
  • +255 719 541 483 / +255 762 291 395

Objectives of the Association

Empowering widowed women through advocacy, training, and community building.

1. Kutetea na kupigania haki za wanawake wajane.

2. Kuwaunganisha wanawake wajane wa umri wowote kutambua matatizo yao na kubuni mbinu za kushinda vikwazo.

3. Kuwatambua wanawake wajane wenye ueledi kwa mafunzo yenye taaluma husika.

4. Kuwahamasisha kukuza vipaji vyao ili wajiingizie kipato halali na kuondokana na utegemezi.

5. Kusimamia na kuishauri jamii juu ya maslahi ya kundi.

6. Kuwasaidia wazee ambao hawajiwezi wenye umri wa miaka 70 na zaidi.

7. Kuwaunganisha wanawake wajane Tanzania bara na visiwani na nje ya nchi.

8. Kuendesha mafunzo, semina, makongamano na vipindi mbalimbali kuhusu masuala ya wajane.

9. Kushirikiana na wizara husika na taasisi mbalimbali za serikali na jamii nyingine.

RECENT POSTS

Programu ya Msaada wa Elimu kwa Watoto wa Wanawake Wajane

Shirikisho la Wanawake Wajane limeanzisha programu mpya ya msaada wa elimu kwa watoto wa wanawake wajane. Programu hii inalenga kutoa misaada ya kifedha kwa watoto wa wanawake wajane ili waweze kujiunga na shule na kupata elimu bora. Misaada hii itatolewa kwa watoto wa shule za msingi na sekondari katika maeneo yaliyoathirika na umaskini.

20 Jan, 2025 Admin

Habari ya Maendeleo ya Wanachama

Shirikisho la Wanawake Wajane linaendelea kutoa msaada wa kisheria na kijamii kwa wanawake wajane katika maeneo mbalimbali. Leo, tulikuwa na mkutano wa mafunzo ambapo wanawake wajane walijifunza kuhusu haki zao za kisheria na namna ya kushiriki katika miradi ya maendeleo. Tunawahimiza wanawake wote kujiunga na vikundi vya msaada ili waweze kufaidika na huduma mbalimbali tunazotoa.

24 Nov, 2023 Admin

Testimonials

What our members say about us

PARTNERS & COLLABORATORS